Mnamo tarehe 6, Desemba 2018 ilitangazwa kuwa benki ya NIC, taasisi yenye historia nzuri ya benki ya rejareja na benki ya CBA, kinara wa uvumbuzi zitaungana kuunda benki mpya yenye nguvu isiyo na kifani, utaalam na upatikanaji rahisi.
Benki mpya ya NCBA imetumia ufanisi wa NIC na CBA kuunda benki ambayo inaleta pamoja mambo mazuri zaidi - uwezo wa hali ya juu wa simbanking, usimamizi mzuri wa uhusiano na wateja, benki ya biashara inayokua, huduma za kifedha zinazokua kama biashara yako inavyokua, na bidhaa bora zenye suluhisho za uwekezaji zinazolingana na mahitaji yako maalum.
Mtandao wetu mkubwa na huduma zetu za kirafiki unamaanisha kuwa wewe ni sehemu ya benki iliyoenea ulimwenguni pote lakini ya kipekee Afrika Mashariki.
Kuwa na uhusiano wa kibinafsi ndio chachu ya kila kitu tunachofanya. Hii ni kwa sababu tunaamini kuwa uhusiano mzuri na wa kweli unajengwa kunapokua na mafanikio ya kila mmoja na kwamba ufahari sio zawadi adimu lakini hupatikana hatua moja kwa wakati. Tunaweka maslahi ya muda mrefu ya wateja na jamii kwanza. Sisi ni benki ambayo itasaidia malengo ya ukuaji wa uchumi wa Kenya na mikoa yake.
Karibu kwenye benki ambayo ipo kwa ajili ya matarajio yako. Karibu kwenye Benki inayosema "Go for it".
Karibu NCBA.
Ratiba za muungano wa NCBA na hatua muhimu.
Disemba 2018
Bodi za NIC na CBA ziliidhinisha kuanza kwa majadiliano juu ya uwezekano wa kuungana.
Januari 2019
Bodi za wakurugenzi za NIC na CBA zilipiga kura kwa kauli moja kupendekeza kwa wanahisa kuunganishwa kwa benki hizo mbili.
Aprili 2019
Wanahisa wa NIC na CBA waidhinisha kuunganishwa kwa benki hizi.
Mei 2019
Mkurugenzi mtendaji wa kikundi na mwenyekiti wa Tanzu ndogo ya Benki ya Kenya ilitangaza uongozi wa chombo kipya.
Septemba 2019
Uidhinishaji ulipokelewa kutoka benki kuu ya Kenya na Katibu wa Baraza la Mawaziri la Hazina ya Kitaifa.
Oktoba 2019
Tunaungana kuwa NCBA.